Siasa Hizi Poem by priscah Mutswenje

Siasa Hizi

Alisema Bifwoli, mwanasiasa shetani
Alinena Wakoli, mwanasiaa mtani
Hukata makali, wakadai si vitani
Huzika wakali, kuondoa mitani

Vigeugeu wanasiasa, mipango tumbitumbi
Hudai sina sasa, ahadi kuteremshia ukumbi
Kwa misemo na visa, huinua nyingi vumbi
waitwe wa kisasa, wa zama huwa pimbi

Hutiumbuiza ikibidi, kuchochea upendo
Na pingamizi ikizidi, Fujo kwa si tendo
Wepesi wa ukaidi, hata kama ni uvundo
Ikiwazidi baridi, humtembelea Loliondo

Wananchi mna kazi, kujasusi na kuchagua
Sipumbazwe na vazi, humsetiri mchagua
Weka kwa makavazi, matendo ukikagua
Changanua yao makazi, na kwao kubagua

COMMENTS OF THE POEM
READ THIS POEM IN OTHER LANGUAGES
Close
Error Success