Dini zetu zote mbili, Imejificha na siri,
Miaka yote miwili, Ijumaa kwetu heri,
Ishirini yenye mbili, Imeonyesha ukweri,
Nikisema jumapili, Watu watanikejeri.
Ijumaa hii ya pili, Imekuja mara mbili,
Ikija na mbili mbili, Kuonyesha jambo hili,
Msipokuwa wawili, Kuzaliwa mara mbili,
Mipango mtagaili, Msipofanya adili.
Sitosema hio siri, Nataka mtafakari,
Ambaye ni jemedari, Ameitambua hari?
Je umeona hatari? Au mambo yote ni shwari?
Kiswahili na shairi, Mmeelewa vizuri?
This poem has not been translated into any other language yet.
I would like to translate this poem