Bukheri wa moyo nimpapo kiazi kikuu
Maana kwa hakika alobobea huipanua ilo finyu
Nami nimepata mzio, tena mzio wa vitu adhimu.
Asofundi maridhawa, kafumua mfumo fumu.
Mie ndio yule dereva alogawa usukani
Mie nikampa Chombo asiyeona asilani
Ashakumu, namkirita sugusugu forodhani
Hakika haoni, ila mie timilifu yake mboni
Nakupeni kongole mlio lilisha vibanzi
Jipu podo podole, usoni lisilo simanzi
Tamaduni kongwe chambile, hilipia dudu mizi
Kongole mlolilea, koroma jumba gongo nazi.
This poem has not been translated into any other language yet.
I would like to translate this poem