Majukwaa ya malimwengu, kaniachia mlimwengu
Nikiwa kinda bovu walimwengu, kaniwingia masaibu
Msichana mwenye mizungu, ndiye marehemu Swaibu.
Mvuto wa sauti, aliiva mamangu, nyimbo zikawa jawabu
Anapita anifurahisha, apendeza, aliangusha mwanga wa kusisimua.
Zikan'gaa nyuso za hadhira, macho yao yakawa tayari,
Kupumbaze walo mathara, hoha hahe kwa pepari
Kuigiza hadharani Sara, alibobea mamangu kama ndoto ilositiri
Mishororo aliimulikia dira, kama mchezo wa kamari
Anapita anifurahisha, apendeza, aliangusha mwanga wa kusisimua.
Stans 2:
Jukwaani aliposimama, kemi na viglegele vilitawala
Akajawa na shamrashamra kudanganywa na kina wala
Milipuko ikamtazama, kwa jicho la uhasidi na balaa
Kaleta dhoruba na lawama, ilobaki kitendawili na jela
Mwisho alikwama, kwa ngoma ya changamoto pewahela.
Milipuko ya fataki, iluiunguza talanta asipendeze jamaa
Stans 3:
Nikasawajika sawasawa, nikadhoofika kiafya, maskini nikalia
Kaumia aso pawa, tama nikashika, mikosi Kusimulia
Umma linibatiza mfiwa, huruma ndo pokezi, hali ngumu linijia
Njaa nikaitambuwa, makiwa nikahojiwa, ushauri nikaingilia
Hakika ulinikombowa, machoni mwa mateso, jukwaa nikapalilia,
Mwongozo kwa talanta, umekuwa ndo yangu njia
Stans 4:
Mchoro wa mawazo, kama upepo unavyochukua majani,
Anachora njia, kueleza kwa ufasaha, sio tu kama fikra za kawaida.
Mishororo inaleta changamoto kuu, kama mlima mkubwa,
Msichana wa talanta, anavuka vikwazo, anashinda siku zote.
Stans 5:
Nipisheni jamani niipige ino ngoma, ya elimu inadai viatu vya maarifa,
Sinitie uwoga naondoa ii lawama, sintofahami po kwa'ko taarifa.
Hadharani anajenga daraja njema, kutoka upwekeni hadi ushindi,
Na kwa ya kale katu sitakwama, kusudi niyashinde hayo maafa
Naendeleza talanta kwangu dawama, tawakilisha nguzo zangu sifa.
Stans 6:
Kuna nuru jamani, Nuru itawaka kama taa inayong'ara gizani,
Nitachonga wani njia uchumi nitatenga na maono pinzani
Kimalenga nitajiauni, sikubali vishawishi ufahamu baruani
Sitegemei vya puani, miundomsingi imejaa mwangu ghalani
Msichana wa talanta, nitachuma kwa ufungua wa mabadiliko.
Stans 7:
Sitegemei miondoko ya kuvutia, nategemea upanzi wa raslimali inavyoendelea
Ushindi wa juani kiuchumia, kwa hoja, mahojiano na tamasha ilobobea
Talanta yangu sitangojea, naipalilia kwa kama kalamu na akili ilokolea
Hadharani nitapalilia, mbolea ninyunyizie na kwa hima nitajitolea.
Naendeleza talanta kwangu dawama, tawakilisha nguzo zangu sifa.
Stans 8:
Sijamaliza kilijonileta lakini ni tamasha, au ni mashindano jamaa?
Uchumi ni akili pevu, wazo za kukesha, siduwai mimi natazama
Uchangani nilitishwa na dhoruba ya Maisha, nilomtegemea lipozama
Nyota ikazima, nikajua kwisha, polepole nikaangaza pa kushika kusimama
Umalenga langu dirisha, melifungua kulikuza tazama talanta yavuma
Usanii kukua, bora umee mizizi ni kujenga uchumi kuendeleza talanta
This poem has not been translated into any other language yet.
I would like to translate this poem