Lenga mishale mwana, lenga tena mikali
Sije kuchoka mwana, kwayo yako makali
Silaha ya kufana, iwe kwako halali
Fuma sijakukana, fuma ilo mikali
Bado mie natamba, natamba nayo hali
Sio kwayo maneno, bali hata matendo
Kukwepa konokono, huuchuja vishindo
na mwema msono, hudhihaki mgando
ushindi ndilo neno, sipendi magendo
Bado mie natamba, natamba kwalo pendo
Kata kwa mtazamo, sitizame vya kando
Lenga kwacho kikomo, situpe pale kando
tumia huo mdomo, silaha iso pindo
Tupa na yaliyomo, sibakize la nondo
Bado mie natamba, natamba kimatendo
Kereketwa sifiche, tema kilo kooni
Maumbile ka cheche, sizime jioni
Rabana si mchache, huzisafisha mboni
kwa yote jikumbuche, kani'mba si shetani
Bado mie natamba, natamba upeoni
This poem has not been translated into any other language yet.
I would like to translate this poem