Angurumapo Simba mcheza nani.
Mambo kangaja hamjui kwani.
Huenda yakaja ilinenwa zamani.
Alesikia keshapata singoje jamani.
Rumba yetu sisi tuicheze kijasiri.
Kunengua hakutoshi lazima ipo siri.
Kupanga mirindimo tufikie kasri.
Alesikia keshapata siambiwe subiri.
Visu hunolewa kabla ya chinjio.
Jogoo huwika kuje chajio.
Yohana litangaza wa Yesu ujio.
Alesikia keshapata sitegemee tarajio.
Ja mkulima jifunge kibwebwe.
Mvuani, juani au kwa kipupwe.
Huangaza ajibiidishe maanake asipitwe.
Alesikia keshapata kesho asipitwe
This poem has not been translated into any other language yet.
I would like to translate this poem